Mkurugenzi mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewataka wafanyabiashara na Wananchi wanaofanya biashara kwenye minada na magulio kulipa ushuru na mapato yanayostahili ili kuboresha miundombinu ya maeneo husika. Akizungumza leo na Timu ya Ukusanyaji mapato kwenye ofisi za Makao makuu ya H/ Wilaya Babati Arri kiongozi huyo amesisitiza " Kila mfanyabiashara / mwananchi anayefanya biashara kwenye minada/ magulio anayesitahili kulipa mapato alipe kwa kiwango kinachostahili" amesisitiza kiongozi huyo.
Mkurugenzi huyo amesisitiza timu ya Ukusanyaji mapato kufanya kazi kwa bidii, kujituma, na kuwa waaminifu katika Ukusanyaji mapato ya Halmashauri ili mapato yanayopatikana ya kamilishe miradi mbalimbali ya Maendeleo.Aidha amesisitiza Kila baada ya mnada/ gulio kumalizika usafi ufanyike mara moja na kuagiza kununuliwa kwa vifaa vya usafi kwa kila mnada na gulio.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.