Naibu waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Eng. Kudo Mathew ametembelea Wilaya ya Babati leo kusikiliza na kutatua kero za Mawasiliano ya simu. Mhe.Naibu waziri akiwa Kijiji cha Imbilili Kata ya Signo H/ Mji wa Babati amesikiliza wananchi na kujionea mwenyewe ukosefu wa mawasiliano na kuagiza kampuni ya Halotel kukamilisha ujenzi wa mnara kabla ya mwezi wa nne mwaka huu , Pia akiwa Kijiji cha Endadment kata ya Gidas H/ Wilaya ya Babati amegundua tatizo ni kubwa la ukosefu wa mawasiliano na kuahidi serikali itajenga mnara kurahisisha mawasiliano katika kata hiyo na kata jirani, aidha akiwa kijiji cha Ufana kata ya Ufana H/ Wilaya ya Babati ameona kuna tatizo la mawasiliano ya Simu kata za Ufana na secheda na kuahidi serikali itajenga mnara kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano ktk kata hizo. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameongozana na Maofisa kutoka Wizara na taasisi zilizoko chini Wizara yake na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.