Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Karolina Mthapula Mtapula amewataka Watumishi wa H/ Wilaya ya Babati kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano ili kuwaletea Wananchi maendeleo. Mtapula ameyasema hayo leo kwenye kikao na Timu ya Menejimenti kilichofanyika katika ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati Arri. " Nyinyi kama Watumishi fanyeni kazi kwa pamoja na ushirikiano ili kuwaletea Wananchi maendeleo " amesisitiza kiongozi huyo .. Wakati huo huo Mthapula ametumia fursa hiyo kupongeza Uongozi ,Madiwani na Watumishi wa H/ Wilaya ya Babati kwa kupata Hati safi kwenye Hesabu za fedha za mwaka 2021/2022. Katibu Tawala Mkoa anaendelea ziara yake ya kutembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara kufuatilia shughuli maendeleo na kutatua changamoto zinazozikabili Halmashauri.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.