Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Joseph Nyamhanga ameagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha fedha zote zilizoletwa kukamilisha ujenzi wa Maboma kwa shule za Sekondari zinatumika kikamilifu kukamilisha ujenzi huo kabla ya tarehe 30,June 2019 vingenevyo fedha hizo zitahamishiwa kwenye Miradi mingine.Katibu Mkuu ameyasema hayo leo Katika Shule ya Sekondari Gichameda iliyoko kata ya Magugu Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi Mkoani Manyara.Akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ametembelea na kukagua Kituo cha Afya Nkait,Kituo cha Afya Magugu,Shule ya Sekondari Gichameda na Ghala la kuhifadhi mazao lililoko katika Kijiji cha Matufa kata ya Magugu ambapo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati,Wakuu wa Idara na Wananchi wote kwa ujenzi na usimamizi na akawaagiza Miradi hiyo waisimamie vizuri,waitunze ili itoe huduma bora kwa Wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.