Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira imepongeza Kata za Arri na Dareda kwa ujenzi na ukamilishaji Madarasa mapema kwa ajili ya mapokezi ya Wanafunzi wa Kidato Cha kwanza mwaka 2023. Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Adamu Ipingika Kwa nyakati tofauti katika Kata ya Arri na Dareda wakati kamati hiyo ikikagua miradi ya Maendeleo. " Kamati imeridhishwa na ujenzi wa Madarasa ya mapokezi ya Kidato cha kwanza mwaka 2023 mapungufu machache yalionekana yarekebishwe " amesisitiza kiongozi huyo. Aidha kamati ikiwa Katika Shule ya Sekondari Dareda iliyoko Kata ya Dareda imepokea ombi la Kata hiyo kuanzishwa Kwa Shule mpya kutokana na eneo la Shule hiyo kuwa dogo na ongezeko la wanafunzi kwa Kila mwaka." Kamati imeagiza Kata hiyo kuweka ombi hilo kwenye Mpango wa Bajeti unaoanza mwezi huu. Aidha kamati imeagiza viti na meza vitengenezwe Kwa vipimo na ubora unaotakiwa. Halmashauri ya Wilaya ya Babati ilipokea Tsh 400 Million kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa 20 ya Mapokezi ya Kidato Cha kwanza 2023
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.