Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Babati wamewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Babati, Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati na viongozi wa Kata ya Secheda kwa utekelezaji vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi. Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Babati Mhe. Jackson Haibei wakati wa majumuisho baada ya ukaguzi wa miradi ya sekta ya maji, Afya, Elimu na Barabara" Kamati ya Siasa inampongeza Mkuu wa Wilaya Mhe. Twange kwa usimamizi na utekelezaji vyema ilani ya CCM , ni kweli usiopingika ilani imetekelezwa katikaH/ Wilaya ya Babati Tunawapongeza" .Mhe. Haibei amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi bora wa Miradi. Kamati ikiwa Shule mpya ya Sekondari Secheda Imepongeza serikali kwa kutoa fedha kiasi cha Tsh 584,280,028/ kujenga shule hiyo mpya ambayo imefunguliwa tarehe 8/1/2024
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.