Kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara imepongeza Wilaya ya Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ujenzi wa miradi mizuri ya maendeleo yenye tija kwa jamii .Hayo ameyasema Mwenyekiti wa cha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Mhe. Simon Lulu Kata ya Bashneti wakati wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Manyara wakikagua Kikundi cha Vijana cha Mahea ikiwa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2015 hadi 2020 " Mkuu wa Wilaya ya Babati na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Tunawashukuru sana kwa utekelezaji wa ilani ya chama kwa Vitendo ,miradi yote iliyotembelewa ina tija kwa jamii" amesisitiza kiongozi huyo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.