Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati umekubali kuanza upya kutekeleza mfumo wa stakabadhi wa ghala mwaka huu ili kuongeza mapato ya ndani. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe.John Noya mara baada ya Mafunzo ya usimamizi wa stakabadhi za ghala yalifanyika leo kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Kuendeshwa na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala." Tunashukuru kwa mafunzo haya na Sisi Madiwani tunakubaliana mfumo huu uanze mwaka huu ili kuongeza mapato ya ndani amesisitiza kiongozi huyo.Aidha amewataka wafanyabiashara kununua mazao kwenye vituo (Makao makuu ya Kata)badala ya kwenda moja kwa moja shambani.Akitoa Mafunzo hayo Kwa Wahe.Madiwani, Wakuu wa Idara na Viongozi wengine, Meneja wa Mipango na Uhamasishaji kutoka Bodi hiyo Ndg Sura Ngatuni amesema mfumo wa Stakabadhi wa ghala unafaida kubwa ikiwa ni pamoja na ongezeko la bei ya mazao,ongezeko la mapato kwa mkulima na Serikali,kichocheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa kwenye soko.Kwa mwaka 2018/19 Halmashauri ilipata faida ktk mfumo huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.