Baraza la Madiwani limempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg Anna Mbogo na Timu ya Menejimenti kwa kupata Hati safi kwa mwaka wa fedha 2021/2022.Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti Mhe. John Noya kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Akiwasilisha Taarifa ya Serikali kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani , Mkurugenzi Mtendaji Ndg Anna Mbogo amesema "Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aliwasilisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa kwa mwaka 2021/2022 katika ripoti hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepata Hati safi" . Ndg Mbogo ameongeza kuwa anawashukuru Madiwani, Viongozi na jamii kwa ushirikiano na kusimamia shughuli za maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.