Halmashauri ya wilaya ya Babati imepata hati safi kwa ukaguzi wa fedha za Mwaka wa fedha 2022/2023. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Godfrey Jafari wakati akiwasilisha taarifa ya Serikali kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri. Ameongeza kuwa ukaguzi huo ulihusisha manunuzi, miradi ya maendeleo, mikataba,mapato na matumizi na masuala ya kiutumishi. Aidha Ndg Jafari amewashukuru Wahe. Madiwani , wenyeviti wa vijiji na vitongoji watendaji , wataalam na wananchi katika kusimamia shughuli mbalimbali zilizopelekea kupatikana kwa hati safi . Naye mwenyekiti wa H/ Wilaya Babati John Noya amepongeza na kusema ushirikiano huo uendelee. Halmashauri ya Wilaya ya Babati imekuwa ikipata hati safi kwa miaka sita mfululizo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.