Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeanza kutoa mafunzo ya ukusanyaji kodi ya Majengo, Pango la Ardhi na ushuru wa mabango kwa Watendaji Vijiji na Kata.Akifungua mafunzo hayo leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Godfrey Jafary amesema Serikali imefanya marekebisho mbalimbali kwenye Sheria ya Fedha Na. 2 ya Mwaka 2023 Mabadiliko hayo yameweka jukumu la kusimamia na kukusanya Kodi ya Majengo, Kodi ya Pango la Ardhi na ushuru wa Mabango utakusanywa na mamlaka ya Serikali za mitaa isipokuwa Majengo yaliyosamehewa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za mitaa ( utozajiwa Kodi za Majengo sura 289. Ndg Jafar amesisitiza washiriki hao mara baada ya mafunzo kwenda kufanya utekelezaji kwanza kwa kutoa Elimu kwa wananchi kupitia mikutano na vikao mbalimbali vya kisheria.Washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru Serikali kwa utoaji Elimu hiyo na kuhaidi kwenda kutekeleza
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.