Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeahidi kutoa Bati kwa ajili ya kumalizia Majengo ya Madarasa ya Shule za Sekondari ambayo yamefikia hatua ya kuweka ya Kupauliwa na kuwataka Madiwani kuharakisha ujenzi ya Majengo hayo.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Iddi Malinga kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mkurungezi huyo amesema amenunua Bati bando 140 zenye thamani ya Milioni Arobaini (40) geji 28 zenye uwezo wa kuezeka madarasa 31 Kwa upande wa Madiwani wamemwomba Mkurugenzi huyo,mgao wa Bati hizo kwa ajili ya kumalizia Nyumba za Walimu na Vyoo vya Wanafunzi katika Shule za Sekondari zenye upungufu huo,ili kuleta hamasa kwa Wananchi wanao changia miradi mbalimbali. Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amesema nia ya Serikali ni kukamilisha vipao mbele muhimu kama vile Madarasa ya Sekondari ili majengo hayo yaweze kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kuingia mwaka 2018.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.