Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara kwa mwaka 2023/2024 imepanga kukusanya kiasi Cha Tsh 3,445,000,000 kutoka mapato ya Vyanzo vya ndani. Wakijadili mapendekezo ya makadirio ya Mpango na Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha2023/2024 leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa siku ya kwanza uliofanyika Ktk ukumbi wa Makao makuu M/ kiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amesema " Halmashauri ni ya kwetu wote Madiwani na Watumishi tuungane pamoja kuhakikisha tunakusanya mapato yote ya Halmashauri kutoka Vyanzo vyote vya ndani" amesisitiza kiongozi huyo . Aidha amesema Hali ya hewa si nzuri lakini tukishirikiana kwa pamoja , Madiwani, mawakala, Watumishi na kutoa Elimu Kwa Wananchi mapato ya yatapatikana na kupanda zaidi. Amesisitiza Kila diwani ktk eneo lake asimamie ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewataka wanunuzi wa mazao kufuata Sheria na taratibu kuhakikisha wanalipa ushuru wa mazao unaotakiwa bila udanganyifu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.