Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles M. Nyerere leo amekagua na kufuatulia ujenzi wa madarasa kwa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 na kupongeza Halmashauri ya wilaya ya Babati kwa hatua ya ujenzi wa madarasa hayo ilipofikia. Hayo ameyasema kwa nyakati tofauti alipotembelea Shule Shikizi ya Kazaroho, Shule ya Sekondari Kisangaji zilizoko kata ya Kisangaji ,Shule ya Sekondari Matufa kata ya Magugu na Shule ya Sekondari Kiru iliyoko kata ya Kiru Halmashauri ya Wilaya ya Babati." Nimefurahi kazi inaendelea vizuri na vifaa vilivyonuliwa kwa fedha za serikali vinatunzwa vizuri, ongezeni juhudi katika ujenzi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati." amesisitiza kiongozi huyo,Katika Shule zote , Mkuu wa mkoa amekagua ujenzi,ulipofikia amekagua vyumba vya kuhifadhia vifaa,nyaraka za kupokea na kutoa vifaa na kujiridhisha maeneo yote yanayojengwa miradi hiyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.