Maofisa ugani Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kuendelea kutoa elimu ya kudhibiti na madhara ya sumu kuvu kila mara. Hayo yamesemwa na Afisa Kilimo Kutoka wizara ya Kilimo Ndg Ester Mwaisango kwenye washa ya kupitia vifungu vya Sheria ndogo ya Kudhibiti sumu kuvu kwa Watendaji wa kata iliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati" Sumu kuvu ina madhara makubwa kiafya na kiuchumi toeni elimu kila mara".Amesisitiza kiongozi huyo. Kwa upande wake Mwanasheria wa H/Wilaya ya Babati Ndg Godfrey Japhari ambaye amewapitisha watendaji kwenye sheria ndogo ya Kudhibiti sumu kuvu amesema watendaji wakisimamia sheria hiyo italeta manufaa makubwa kuanzia kuvuna, kuhifadhi mpaka kusafirisha mazao yao. Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa H/ W ya Babati Ndg Benedict Ntabagi amesema sheria ndogo waliopitia imekamilika hivyo kila mtendaji atoe elimu kwenye mikutano ya kijiji hadi kata ili wananchi waelewe na akatoa shukurani kwa Wizara kuleta mradi wa kudhibiti sumu kuvu katika H/Wilaya.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.