Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Lazaro Twange ameomba taasisi mbalimbali kushirikiana na Madiwani wa Halmashauri Wilaya Babati katika kuwaletea wananchi maendeleo. Hayo ameyasema leo kwenye kikao kazi cha Madiwani wa H/Wilaya ya Babati, taasisi za TANESCO, RUWASA, BAWASA na TARURA kilichofanyika katika ukumbi wa H/W_ Babati." Tumeitana hapa kufafanua hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika trh 4/11 ambapo baadhi ya madiwani walitoa hoja na kutaka ufafanuzi zaidi kutoka baadhi ya taasisi " amesisitiza kiongozi huyo.Akijibu baadhi ya hoja mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe Daniel Sillo amesema Mradi wa Maji Darakuta hadi Minjingu utakamilika Juni 2024. Naye Mwenyekiti wa H/W -Babati Mhe. John Noya amesema Madiwani wanapokwenda kwenye taasisi mbalimbali wanatakiwa kusikilizwa kwani wao ni wawakilishi wa Wananchi. Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara, Meneja TARURA, RUWASA, TANESCO ambao wametoa taarifa za utekelezaji wa kazi zao .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.