Wananchi wa kata ya Qameyu Halmashauri ya Wilaya ya Babati wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emanuela Kaganda kwa kwenda kuwasikiza na kutatua kero za wananchi. Wananchi hao wameyasema hayo leo kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya wa kusikiliza na kutatua kero uliofanyika makao makuu ya Kata hiyo. '" Sisi wananchi tumefurahi na tunakupongeza kwa kuja,kusikiliza na kutatua kero zetu kwa umakini tunakupongeza sana" . Mhe. Kaganda amesisitiza wananchi hao kupendana kushirikina na kuishi kwa amani na kuacha uongo na uzushi. Sambamba na hilo amesisitiza wananchi ambao bado hawajapeleka watoto kuripoti kidato cha kwanza wahakikishe wanawapeleka watoto hao haraka mwisho wiki hii baada ya hapo hatua kali zitachukuliwa. Aidha ameagiza Halmashauri kupitia idara ya Wanyapori kwenda kata ya Qameyu kutoa Elimu ya kufukuza Tembo dhidi ya kuharibu mazao yao.Mhe. Kaganda ameendelea kutembelea Kila Kijiji kusikiliza na kutatua Kero ikiwa na kuhamasisha usimamizi na ujenzi miradi ya maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.