Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Jacob Twange amewataka Watumishi wanaokwenda kuhakiki kaya Masikini kuwa waaminifu na kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa ili kuwezesha mradi wa TASAF awamu ya tatu kufanikiwa. Hayo ameyasema leo akifungua mafunzo kwa Wakuu Idara na Wawezeshaji wa H/Wilaya ya Babati yaliofanyika ktk Ukumbi wa H/Wilaya ya zamani" Siku zote rasilimali ni chache hazitoshi,nendeni mkafanye kazi kwa uaminifu na mzingatie miongozo ili anayetakiwa kupata apate na si vinginevyo". Amesisitiza kiongozi hiyo.Mafunzo hayo ya kujenga uelewa yameanza leo na yatamalizika trh 14/7 na baada ya Mafunzo hayo kazi ya kwenda Vijijini kuhakiki kaya masikini itaanza.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.