Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati Ndg Halfan Matipula amesisitiza Watumishi wa H/ Wilaya ya Babati kuendelea kufanya kazi Kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo. Hayo ameyasema leo kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa H/Wilaya ya Babati. "Tunapovunja Baraza la Madiwani hatuna budi kusisitiza Timu ya Menejiment kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo.Amesisitiza kiongozi huyo Ametumia muda huo kuwashukuru Wahe Madiwani wote, Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo na Watumishi wote kwa mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha miaka 5 na kuwaomba ushirikiano uendelee . Kwa Upande wake Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati amesema wao wanaondoka lakin wameacha H/ Wilaya Babati iko mikono salama ya Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo, Wakuu wa Idara na kusisitiza mazuri yote na mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha Miaka 5 yaendelezwe .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.