Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limepongeza Walimu na Wanafunzi kwa kufanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa kumalizia Elimu ya Msingi na Elimu Sekondari kwa mwaka 2023 .Pongezi hizo zimetolewa leo na Mhe John Noya M/Kiti wa Baraza hilo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wakati wa kujadili Taarifa ya utekelezaji kwa robo ya pili inayoishia mwezi Desemba 2023. "Tunawapongeza Mkurugenzi, Walimu na Wanafunzi wa H/Wilaya kwa kufanya vizuri katika mtihani ongezeni juhudi na mwaka huu wa 2024 amesisitiza kiongozi huyo .Awali Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo ameliambia Baraza la Madiwani kuwa matokeo ya kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2023 waliofaulu ni 7811 sawa na asilimia 82.40 na Matokeo ya Kumaliza kidato cha nne mwaka 2023 waliofaulu walikuwa 3,131 sawa na asilimia 99.46.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.