Baraza la Madiwani la H/ Wilaya ya Babati limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha kiasi Cha Tsh 400,000,000/ nje ya bajeti ya H/ Wilaya kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya mapokezi ya Kidato Cha kwanza mwaka 2023.
Akizungumza leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati baada ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,Ndg Benedict Ntabagi kuwasilisha taarifa ya mapokezi ya fedha kwenye Mkutano wa Baraza hilo. Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya amesema "Sisi Baraza la Madiwani wa H/Wilaya ya Babati tunampongeza sana Mhe. Rais kwa kutoa fedha Kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya kuwapokea wanafunzi wa Kidato Cha kwanza mwaka 2023" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha Mkurugenzi Mtendaji amelieleza Baraza hilo kuwa H/ Wilaya ya Babati pia imepokea fedha kiasi Cha Tsh 889,250,000 / Kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo na miradi itakayotekelezwa Kwa fedha hizo imewasilishwa kwenye Mkutano wa Baraza hilo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.