Baraza la Madiwani la H/W Babati limempongeza Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kwa kazi nzuri aliyoifanya ya maandalizi, kusimamia na kushiriki kufanikisha shughuli za mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika H/Wilaya na Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa. Akitoa pongezi hizo leo kwenye Mkutano wa Baraza uliofanyika makao makuu, Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya amesema Mkuu wa Wilaya amefanya kazi kubwa ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge kwa Halmashauri na kilele cha mbio za Mwenge kitaifa ambacho kilifanyika katika Wilaya ya Babati. Akipokea pongezi hizo , Mhe. Twange ameshukuru sana na kusema pongezi hizo ni kwa viongozi wote wa Wilaya ya Babati kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya ambao ameshirikiana nao kufanikisha maandalizi ya hayo . Wakati huohuo Mhe. Twange ameagiza madiwani kuendelea kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao " Tunayo miradi mingi inayotekelezwa kwenye kata zenu simamieni ikamilike kwa wakati na ianze kutoa huduma " amesisitiza
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.