Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati limepongeza shirika la So they can (STC)kwa ujenzi wa miradi inayotoa matokea chanya kwa wananchi. Akiongea kwenye mkutano wa Baraza laMadiwani leo kwenye kikao cha kwanza cha kujadili Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya amesema anafurahishwa na mpango na Bajeti wa shirika hilo uliowasilishwa kwenye Baraza hilo kuwa utatoa matokeo mazuri kwa wananchi." "Tunawashukuru sana kwa miradi iliyoanzishwa na kutekelezwa na shirika lenu Tarafa ya Babati asanteni sana ushirikiano huo uendelee " amesisitiza kiongozi huyo.Shirika la So they Can lenye makao makuu Mjini Babati limejikita sana katika uboreshaji miundombinu ya shule,kuwaendeleza walimu,Elimu ya kilimo cha Bustani shuleni,kufadhili wanafunzi kwenye masomo. Kwa mwaka wa fedha 2025/2026 shirika hilo linategemea kutumia Tshs 2.2 billion katika kutekeleza miradi mbalimbali katika shule za Msingi 29 na shule za sekondari 5 kwa kata za Endakiso, Mamire, Qash na Gallapo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.