Halmashauri ya Wilaya Babati imeagiza Bajeti zinazoandaliwa Kwa mwaka 2024/2025 zishirikishe wananchi ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa wananchi. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg Benedict Ntabagi kwenye mafunzo ya watendaji wa kata na vijiji kwa ajili ya maandalizi ya Mipango na Bajeti kwa Mwaka 2024/2025 kilichofanyika leo katika ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati. " Mipango yote ya Bajeti lazima ianzie ngazi za chini hivyo mnatakiwa kushirikisha wananchi kuanzia huko ili wananchi wailewe na kuitekeleza" amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo Ndg Ntabagi amesisitiza watendaji hao kufanya kazi kwa bidii kutatua kero za wananchi na kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya H/!Wilaya ya Babati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.