Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imetoa tuzo kwa Wild Impact (Africa Foundation) na Beyond Lake Manyara Tree Lodge Wadau wa maendeleo kwa kuthamini mchango mkubwa wa katika kuboresha Elimu. Tuzo hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa H/Wilaya ya Babati Mhe.John Noya kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo kwenye ukumbi wa H/Wilaya. "Kila mwaka tunatoa tuzo kwa wadau wa maendeleo kwa kuthamini mchango mkubwa wa maendeleo katika Taasisi yetu." Kwa mwaka 2023/2024 tunapongeza na kuthamini mdau Wild Impact (Africa Foundation )na Beyond Lake Manyara tree Lodge kwa ujenzi wa miundombinu ya shule ya Sekondari The Tara Getty iliyoko kata ya Magara" Amesisitiza kiongozi. Akipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Wadau hao, Mkuu wa shule ya Sekondari The Tara Getty Laptan Mollel ameshukuru H/Wilaya kwa kuthamini mchango wa wadau katika ujenzi wa shule hiyo na kuahidi mahusiano mema na taasisi yake.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.