Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeteuliwa kuwa ya mfano kitaifa kwa utoaji wa chakula cha mchana mashuleni. Getrude Kavishe Afisa Elimu Shule za Msingi ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati uliofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano " H/ Wilaya ya Babati kwenye Takwimu za Kitaifa ni kati ya Halmashauri ya 3 ;zenye zaidi ya asilimia 80 uchangiaji mkubwa wa chakula wa wazazi na utoaji chakula mashuleni".Wakati huo huo Bi Kavishe amelieleza Baraza kuwa Wizara ya Elimu , Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na mdau wa maendeleo GAIN wameichagua H/ Wilaya ya Babati kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa utoaji chakula mashuleni ambao utatumika katika nchi nzima. Naye M/Kiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amepongeza Madiwani kwa utekelezaji wa chakula mashuleni na Wizara ya Elimu na ofisi ya Rais TAMISEMI kuchagua H/ Wilaya Babati kuandaa mwongozo kitaifa juu ya utoaji chakula mashuleni
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.