Afisa Mwandikishaji Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewataka waandikishaji kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura kujituma , kufanya kazi Kwa bidii kuhakikisha zoezi la Uboreshaji Daftari la Kudumu Awamu ya Pili linafanikiwa. Afisa Mwandikishaji ameyasema hayo leo kwenye ufunguzi wa Mafunzo kwa waandikishaji yaliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa ya Shule ya Sekondari ya Ayalagaya. "Tunaanza uboresha Daftari la kudumu Awamu ya pili , fanyeni kazi hiyo kwa umakini. na uaminifu" amesisitiza kiongozi huyo . Wakati huo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kwenda kwenye vituo walivyojiandikisha Mwaka jana kuhakiki Majina yao kwenye Daftari ambalo limewekwa wazi. Zoezi la Uboreshaji Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa Halmashauri ya Wilaya Babati litaanza tarehe 16. 5 na kumalizika tarehe 22.5 wananchi wote wenye sifa wanaombwa kwenda kushiriki
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.