Wananchi wa Kata ya Magugu H/ Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Sarame katika kata yao. Hayo yamesemwa na Wenyeviti wa Vitongoji leo kwa nyakati tofauti mbele ya kamati ya fedha,Mipango na uongozi kwenye ukaguzi wa miradi ya Maendeleo. " Sisi kwa niaba ya Wananchi tunashukuru Serikali kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Sarame ktk kata yetu itapunguza msomgamano wa wanafunzi ktk Shule mama ya Magugu" wamesisitiza viongozi hao. Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe.John Noya amesisitiza wananchi kuendelea kuchangia ili kuonesha jitihada za jamii katika mradi huo.
Serikali imetoa fedha kiasi Tsh 470 Millioni katika ujenzi wa shule hiyo na ujenzi unaendelea. Shule ya Sekondari ya Sarame inajengwa katika kijiji cha Sarame kata ya Magugu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.