Wananchi Mkoa wa Manyara wametakiwa kupaza sauti ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia. Akihutubia Wananchi kwenye kilele Cha Kampeni ya kutokomeza ukeketaji Mkoa wa Manyara, iliyofanyika leo Kijiji Cha Mandi Kata Dabil H/ Wilaya ya Babati, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe Lazaro Twange ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amesema Wananchi wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kupaza sauti kuanzia ngazi ya Kijiji Kata mpaka Wilaya serikali yao itawasikiliza na itachukua hatua stahiki dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani haitavumilia vitendo vya ukatili wa kinsia hivyo Kila mmoja anatakiwa kujiepusha navyo" amesisitiza kiongozi huyo. Naye Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Ndg Karolina Mthapula amesema Kabla ya kilele Cha Kampeni hiyo wametembea Wilaya zote za Mkoa wa Manyara wamakutana na Wananchi na viongozi mbalimbali kuhimiza Wananchi kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia . Katibu Tawala huyo amesisitiza wazazi/ walezi kutovumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia mara vinapotokea watoe taarifa mara moja kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.