Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Uboreshaji Daftari la kudumu la Wapiga kura Awamu ya Pili. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Anna Mbogo ambaye pia ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Babati Vijijini leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano " Zoezi la Uboreshaji Daftari Awamu ya Pili kwa Halmashauri yetu litaanza tarehe 16 hadi 22/5/2025 . Wah. Madiwani msaidie kuhamasisha wananchi ambao bado ili waboreshe taarifa zao amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amesisitiza Wananchi kwenda kukagua Daftari la awali la kudumu la Wapiga kura ambalo litawekwa wazi kwa kila kituo kilichoandikisha. Halmashauri ya Wilaya ya Babati itakuwa na vituo 36 vya uboreshaji na na vituo hivyo vitakuwa ngazi ya Kata na vitafunguliwa Kila Siku kuanzia saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni Kwa muda wote wa Siku 7
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.