• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Babati District Council
Babati District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango Ufuatiliaji na Takwimu
      • Ardhi mali Asili na Wanyamapori
      • Maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mazingira na Usafi wa Mazingira
      • Afya
    • Vitengo
      • Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ufugaji nyuki
      • Teknologia ya Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Uchaguzi
    • Link ya Machapisho ya Idara/Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kiofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TAWA YAMWAGA MABILIONI BABATI, SHUGHULI ZA UTALII ZANEEMESHA WANANCHI

Posted on: November 16th, 2023

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) katika kipindi cha mwaka 2022/23 imetoa zaidi ya Billioni Mbili kwa Halmashauri ya wilaya ya Babati na Jumuhiya ya Uhifadhi ya Wanyamapori Burunge (JUHIBU) ikiwa ni kurejesha kwa jamii faida zitokanazo na shughuli za utalii zinazofanywa na TAWA wilayani humo.

Hayo yamesemwa Novemba 15, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo itokanayo na gawio linalopatikana kutokana na shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha iliyofanywa na TAWA Mkoani Manyara


"Pato linalopatikana kutokana na shughuli za uhifadhi pamoja na makato mengine yanayosambaa maeneo mengi, kiwango kikubwa sana kinarudi kwa wananchi" amesema


"Kwa mfano siku za hivi karibuni hii Jumuhiya ya hifadhi ya Wanyamapori Burunge iliyopo hapa kwangu Babati wamepata zaidi ya Shillingi Bilioni mbili ambazo zimegawanywa katika vijiji vyote kumi" ameongeza


Mhe. Lazaro amesema kutokana na fedha hizo zipo Zahanati zimejengwa mpaka zimetimia na kuwekewa vifaa tiba pia miradi mingine kama nyumba za waganga, mabweni katika shule ya Sekondari Mbugwe na miradi mingine mingi


Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ameipongeza TAWA kwa kazi kubwa inayofanya wilayani humo kiasi cha kupelekea ujangili  kupungua kwasababu wananchi wanaona manufaa ya moja kwa moja yanayotokana na shughuli za uhifadhi na utalii


Naye Mkurugenzi wa H/W ya Babati Anna Mbogo amesema kupitia mapato ya utalii wa picha na uwindaji wa kitalii asilimia kumi ya mapato hayo huwa inarudi katika ngazi ya Halmashauri na asilimia 65  inapelekwa katika Jumuhiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge ambayo ina jumla ya vijiji kumi na asilimia 25 kubaki TAWA, ambapo fedha hizo hutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya jamii


Akifafanua mgawanyo wa fedha hizo, Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amesema katika kipindi cha Mwaka 2022/23 Halmashauri ya wilaya ya Babati ilipata zaidi ya Millioni Mia tatu na Jumuhiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge zaidi ya Bilioni Mbili fedha ambazo zimetokana na shughuli za utalii.


Aidha  amewaomba wananchi kushirikiana na Mamlaka hiyo katika ulinzi wa rasilimali za Wanyamapori ikiwemo kulinda na kutunza mazingira kwani pasipo uhifadhi imara shughuli za utalii zitazorota na hivyo kulikosesha Taifa pato ambalo lingeweza kuongeza miradi mingi ya maendeleo katika jamii mbalimbali nchini.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA September 25, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 03, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WASIMAMIZI VITUO VYA WAPIGA KURA June 30, 2025
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2020 June 17, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Jamii Imetakiwa Kutumia Vyakula Vyenye Virutubisho

    June 24, 2025
  • DAS Matipula. Watumishi Fanyeni Kazi Kwa Bidii

    June 20, 2025
  • Madiwani Waishukuru Serikali Kwa Ujenzi Wa Jengo La Makao Makuu Ya Halmashauri

    June 20, 2025
  • Mkurugenzi Apongezwa Kwa Utendaji Kazi Mzuri

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

MAKALA YA ELIMU IKIANGAZIA SWALA LA TAALUMA NA HALI YA UFAULU KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BABATI
video zaidi

Viunga vya haraka

  • Watumishi portal
  • Lgrcis dashborad
  • Salary silpportal
  • Ramani ya Halmashauri

Tovuti Mbalimbali

  • Tovuti ya Ofisi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Ofisi ya Raisi,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Wilaya Ya Kiteto
  • Secretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya wilaya ya Babati

    Anwani: P.O BOX 400, Babati.

    Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011

    Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577

    Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani Ya Tovuti

Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.