Wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ayatsea iliyoko kata ya Gallapo H/Wilaya ya Babati mkoani Manyara wakifurahia madarasa yao yaliyojengwa na serikali kwa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19. Madarasa ya mpango huo katika H/Wilaya ya Babati yamekuwa kichocheo kwa wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza kufika kwa wakati shuleni kuanza masomo yao lakini yamekuwa kivutio kwa wazazi pamoja na wananchi kuona madarasa hayo wanapowapeleka wanafunzi kuanza kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na kupongeza Serikali kwa ujenzi wa Madarasa hayo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.