Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Mhe.Daniel Baran Sillo amewezesha shule 5 na Zahanati 2 za H/ Wilaya ya Babati kupata bati 600 kutoka Bank ya NMB . Akikabidhi bati hizo leo kwenye Viwanja vya H/Wilaya Babati ya zamani kwa viongozi wa kata zenye shule na zahanati hizo Mhe. Sillo ameishukuru bank ya NMB kwa kutoa bati hizo na akaomba ushirikiano wa kusaidia jitihada za jamii uendelee. Akipokea bati hizo Diwani wa kata ya Ufana Mhe Benard Bajuta kwa niaba ya Wananchi na Viongozi wa kata zingine ameshukuru kupokea bati hizo kutoka kwa Mbunge kuwa zitasaidia kukamilisha vyumba vya madarasa na Zahanati.Shule na Zahanati zilizopokea bati hizo ni Zahanati ya Tsamas,Zahanati ya Luxmanda, Maabara Shule ya Sekondari Boay , maabara Shule ya Sekondari Kisangaji ,zingine ni Shule ya Msingi Kambi, Datar na Yerotonik za H/Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.