Kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi Wilaya ya Babati vijiji imepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati, TARURA na RUWASA kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Babati vijiji Mhe. Jackson Haibei leo kwa nyakati na maeneo tofauti wakati wa ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo. " Chama kimeridhishwa na utekelezaji mzuri wa Miradi yote Tuliopitia. Tunawapongeza Mkuu wa Wilaya , Mkurugenzi Mtendaji , Meneja TARURA Meneja RUWASA wananchi Kwa utekelezaji mzuri wa Ilani , miradi yote ni mizuri kasi ya ukamilishaji iongezwe amesisitiza kiongozi huyo Miradi iliyotembelewa na Kamati ya Siasa ni Ujenzi wa Vyumba 3 vya madarasa na Matundu 6 ya Vyoo katika Shule ya Msingi Mandagew kata Bashnet, ukaguzi wa mradi wa Barabara ya Ngorongoro Qameyu Utwari Kwa kiwango Cha Changarawe,kata ya Madunga na Qameyu, ujenzi wa mradi wa Maji Kijiji Cha Utwari na Ukaguzi wa kituo Cha Afya kata ya Gallapo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.