Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la H/ Wilaya ya Babati wameomba stahiki za Watumishi kuzingatiwa katika kipindi hiki Cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2023/2024 Wajumbe hao wameyasema leo kwenye kikao Maalumu Cha Baraza hilo Cha kujadili makisio ya Mpango na Bajeti kilichofanyika ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati " Tunaomba Wakuu wa Division na Vitengo wakati wa maandalizi ya Bajeti wakumbuke stahiki za Watumishi ambazo ni Likizo,matibabu, uhamisho, na upandaji vyeo" wamesisitiza wajumbe hao. Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Ktk kikao hicho Ndg Hosea Madama amesisitiza wajumbe hao kwenda kuhamasisha Watumishi kufanya kazi Kwa bidii, kuzingatia maadili na taaluma zao ili kuhakikisha wanawaletea maendeleo Wananchi. Baraza la Wafanyakazi la H/ Wilaya ya Babati linaundwa na Wakuu wa Division, Vitengo na wawakilishi wao,Vyama vya Wafanyakazi na wawakilishi wao ambayo ni CWT, TUGHE,TALGWU ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.