Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. David Silinde amesema Serikali haitaruhusu mwananchi yeyote kukwamisha miradi ya Maendeleo inayojengwa nchini. Mhe, Naibu Waziri ameyasema hayo leo Mkoa wa Manyara ktk Halmashauri ya Wilaya Wilaya ya Babati Kata ya Riroda katika Shule ya Sekondari Chief Dodo kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua Miradi ya Maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Babati akitoa ripoti utekelezwaji Miradi ya Maendeleo
Awali Mkuu wa Wilaya Babati Mhe. Lazaro Twange ameeleza kuwa kuchelewa kwa miradi huo kulikuwa na ugumu kwa Wananchi wa Kata ya Riroda kupokea na kuchangia ujenzi wa Mradi wa Mabweni mawili pamoja na kwamba Serikali imetoa Milioni 160 kukamilisha ujenzi wa Mabweni hayo kwa kigezo cha kutosomewa taarifa ya Mapato ya Matumizi ya ujenzi wa vyoo ktk shule hiyo.Mhe Naibu Waziri amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Twange kwa kazi kubwa ya kuhamasisha Wananchi mpaka wakakubali kupokea mradi huo, kisha Naibu Waziri akaagiza Watendaji nchi nzima kuhakikisha wanasoma taarifa za Mapato na Matumizi ya Michango na miradi yote inayotekelezwa ktk maeneo yao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.