Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Eng. Raymond Mushi ameagiza kila kata kutambua fursa zilizopo kwenye kata zao ili kuanzisha viwanda vya Kati na vidogo Katika maeneo yao. Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo kwenye kikao cha chá kamati ya Ushauri chá Wilaya kilichofanyika ktk ukumbi wa H/W ya Babati."H/W ya Babati inatarajia kuanzisha viwanda vipya 15 kwa mwaka huu hivyo ni wajibu wa kila moja kitambua fursa zinazopatikana ktk kata yake ili kuanzisha kiwanda" amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Aidha Mkuu wa Wilaya amesisitiza uhifadhi wa vyanzo vya Maji na usafi wa mazingira kwa ujumla na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwa kata ambazo bado hazijakamilisha.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.