Wananchi wa kata ya Dabil Tarafa ya Bashnet katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kukamilisha ujenzi Madarasa katika shule ya Sekondari Maganjwa ili iweze kufunguliwa mwezi Januari 2019 na kuwapunguzia hadha wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu kufuata Elimu. Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Cresent Khaday wakati Kamati hiyo ilipotembelea kijiji chá Maganjwa na akukagua shule hiyo ."Viongozi mnatakiwa kuhamasisha na kukusanya michango kutoka Kwa wananchi ili kukamilisha ujenzi wa madarasa ili shule hii ifunguliwe mwezi Januari 2019" amesisitiza Mwenyekiti huyo.Akisoma taarifa ya ujenzi huo Mtendaji wa kata ya Dabil Emilini Mtambo amesema Ujenzi huo ulianza mwaka 2010/2011 lengo likiwa wanafunzi wasome karibu kuliko kutembea zaidi ya Km 7 hadi 10 kufuata shule ya Sekondari mama ya Dabil. Shule hiyo ina madarasa 2 yamekamilika na Madarasa 3 yako hatua ya ukamilishaji. Aidha kamati hiyo imetembelea maeneo ya uwekezaji ya Ziwa lá Chumvi Gidewari, Kilimo cha Kahawa kata ya Arri, Ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Gajal kata ya Ayalagaya na kufuatilia Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati pia kamati hiyo imekutana na Viongozi na wananchi mbalimbali na kuwasikiliza
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.