Wakulima wameshauriwa kulima Mazao yenye masoko ya kibiashara ili waweze kujipatia faida na kuongeza kipato. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mh Elizabeth Kitundu kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati uliofanyika léo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mhe Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo baada ya Afisa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Jetrida Kyekaka kutoa taarifa ya mwelekeo wa kilimo kwa msimu wa Mwaka 2018/2019 unaoanza mwezi Novemba mwaka huu. "Waheshimiwa Madiwani kama mlivyosikiliza taarifa ya Afisa Kilimo na Ushirika wahamasishe wananchi katika maeneo yenu walime, Pamba, Pareto, Kahawa, Maharage machanga ,Mahindi , mihogo na Miwa ambayo ni mazao ya kimkakati, yanafaida na yanasoko lá ndani na nje ya nchi" amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Diwani wa Kata ya Kisangaji Mhe. Adam Ipingika naye ameomba Timu ya Maofisa Kilimo kutembelea kila kata kuhamasisha kilimo cha Maharage machanga kwani zao hilo lina soko hapa nchini na nchi jirani ya Kenya. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hamisi Malinga amesisitiza Wananchi wa Tarafa ya Mbugwe kulima kwa Wingi zao lá Pamba na Miwa kutokana na kuwa na bei nzuri na kufunguliwa kwa Kiwanda cha kuchambua Pamba chá Hanang Cotton Mill na Kiwanda cha Sukari chá Manyara Sugar yeyote viko kata ya Magugu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.