Wafadhili wa shughuli za maendeleo wa Shirika la Water Aid kutoka Canada wameipongeza Serikali ya Tanzania na Wananchi kwa kufanya kazi pamoja na ushirikiano mkubwa ili kujiletea Maendeleo. Hayo yamesemwa na Ndg David Mclnnes Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Water Aid Canada na Kiongozi wa Masafara waliotembelea Tanzania Mkoa wa Manyara Wilaya ya Babati Kata ya Ayasanda Kijiji cha Endanachani kufuatilia, kukagua na kuona mradi wa Maji uliofadhiliwa na Shirika la Water Aid. "Tumetembelea Mradi wa Maji wa Endanachan tumeona na tumeridhika kuwa unafanyakazi na wananchi wamenufaika na Mradi huo tunawashukuru" Amesisitiza Kiongozi huyo. Aidha wafadhili hao wamewaomba wananchi kutunza miradi hiyo kwa maendeleo yao ili kijikwamua katika umasikini. Benitho Kavenuke kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amewashukuru wafadhili hao na kuwaomba kuendeleza kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Ziara hiyo waliongozana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mhe Nicodemus Tarmo na Baadhi ya wakuu wa Idara, Viongozi na wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.