Serikali Wilayani Babati imepanga Kutatua changamoto wanazokabiliana nazo Wanawake wajasiliamali katika kukuza shughuli zao za ujasiliamali na kujiongezea kipato. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng Raymond Mushi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kiwilaya Tarafa ya Mbugwe kata ya Mwada.Kabla ya Hotuba , Mgeni Rasmi amekagua Kazi /shughuli wanazofanya wanawake na kuwapongeza kwa kuendeleza shughuli za ujasiliamali na kukuza viwanda. Aidha Mgeni Rasmi ameongoza Wananchi kupima Afya zao. (picha Matukio Siku ya Wanawake)
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.