Jamii imetakiwa kuacha ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake ili kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla. Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Idd Malinga kwenye mafunzo kwa Kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto ambaye yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. "Ukatili kwa Wanawake na Watoto haikubaliki lazima jamii ichukue hatua dhidi yawanaofanya vitendo hivyo"amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji. Aidha amesisitiza jamii kuhakikisha Mama na Mtoto wanatendewa inavyostahili katika jamii na kuacha mfumo dume.Mratibu wa World Vision Kanda ya Magugu Ndg.Majid Mfinanga amesema kamati hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ni muhimu Sana kwa kuibua na kuandaa mpango wa kuzuia Ukatili kuanzia ngazi ya Kijiji. Mafunzo kwa kamati hiyo yanaendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kushirikiana na Shirika la World Vision Kanda ya Magugu na kuhudhuriwa na Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Wanawake na Watoto kutoka Tarafa za Babati, Gorowa ,Mbugwe na Viongozi wa serikali na madhehebu ya dini.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.