Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Nicodemus Tarmo amewataka Wananchi wanaozunguka Mashamba ya Wawekezaji kulinda usalama na kuwa na mahusiano mazuri kati yao na Wawekezaji wa mashamba makubwa ili wafanye kazi zao kwa ufanisi. Mwenyekiti huyo ameyasema leo mbele ya Wawekezaji na Serikali za Vijiji vya Kiru ndogo, Kimara,Kirudick na Kiru Six Kata ya Kiru kwenye ziara ya kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingara ya Baraza la Madiwani wakati wa ukaguzi wa miradi ,shughuli na vyanzo vya mapato ya H/W ya Babati " Sisi Baraza la Madiwani tunataka Mashamba makubwa yazalishe na yalipe kodi stahiki kwa Serikali hivyo ni lazima Wawekezaji wahakikishiwe usalama" amesisitiza kiongozi huyo.Naye Mwekezaji wa shamba la Miombo Estate Ndg Latif Selemani amewashukuru Madiwani hao na kusisitiza yuko tayari kushirikiana na serikali kwa kazi zote.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.