Mkuu wa Wilaya ya Babati ameagiza kata ambazo hazijakamilisha ujenzi wa Maabara kushirikiana na Wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi wa Maabara za Shule za sekondari kuanzia sasa.Hayo ameyasema leo kwenye Kikao cha Wadau wa Elimu wa H/Wilaya ya Babati kilichofanyika ktk ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Babati day. "Kata ambazo hazijakamilisha ujenzi wa Maabara zianze Mara moja ujenzi huo kwani Masomo ya Sayansi kwa vitendo ni muhimu sana ktk wakati huu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.Amesisitiza kiongozi huyo.Katika Kikao hicho Wadau wameshukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwapatia Vitabu vya kufundishia na Vifaa vya Maabara. Shule za msingi na Sekondari zilizofanya vizuri ktk mtihani mwaka 2019 zimepatiwa zawadi ya cheti cha ushindi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.