Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng. Raymond Mushi leo trh 28.2 amepokea Madawati 47 yenye thamani ya Tsh. 5,000,000 kutoka Bank ya NMB tawi la Babati na kuyagawa Chuo cha Ualimu Mamire kilichoko kata ya Mamire Tarafa ya Babati ktk H/W ya Babati .Akikabidhi Madawati hayo Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Ndg Straton Chilongola amesema kila mwaka wanatoa faida wanayopata kusaidia Jamii, kwani ni kupitia Jamii hiyo ndipo wateja wa NMB wanapotokea hivyo ni wajibu wao kuwasaidi.Katika hotuba yake, Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya amesisitiza Wanachuo kuyatunza Madawati hayo na kusoma kwa bidii ili Elimu hiyo iwasaidie kuwa na Maisha Mazuri na kujenga nchi yao na kuepukana na kufanya vitendo vibaya vitakavyoharibu heshima yao na Chuo pia. Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa H/W ya Babati Ndg Hamisi Malinga, Mhe, Diwani wa kata mamire,Meneja wa NMB Babati,Ndg Francis Kasili, Wakufunzi na Viongozi Mbalimbali Kata na Vijiji.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.